Pata taarifa kuu
ULAYA

COVID-19: WHO yaitaka Ulaya 'kuungana' ili kuharakisha chanjo

Ulaya inapaswa "iungane" ili kuharakisha kampeni yake ya chanjo dhidi ya COVID-19 kwa msaada wa maabara zote, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Afya Duniani, WHO, barani Ulaya amesema.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Hans Kluge amekikiri kuwa 'ana wasiwasi' juu ya hatari ya aina mpya ya kirusi cha Corona juu ya ufanisi wa chanjo.

"Lazima tujiandae" kwa mabadiliko mengine ya matatizo ya virusi, hasa kwa kuimarisha zaidi mpangilio, pia amesema Hans Kluge, mkurugenzi wa kikanda wa shirika la Afya Duniani, katika mahojiano na shirika la habari la AFP.

Wakati huo huo shirika la Afya Duniani, tawi la Ulaya limeonya kuwa janga la virusi vya Corona limeathiri vibaya matibabu ya saratani, huku huduma za saratani zikivurugika katika theluthi moja ya nchi za kanda hiyo.

Akizungumza ljana Alhamisi katika Siku ya Kimataifa ya kupambana na Saratani, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO barani Ulaya Hans Kluge alionya kuwa athari ya janga la Corona kwa ugonjwa wa saratani barani Ulaya ni janga kubwa.

Kluge amesema baadhi ya nchi zinashuhudia uhaba wa dawa za saratani zikiwemo nchi zenye utajiri wa raslimali.

Miongoni mwa mataifa 53 wanachama wa WHO barani Ulaya, ambayo ni pamoja na nchi kadhaa

za Asia ya Kati, moja kati ya nchi tatu imeshuhudia kuvurugwa kwa sehemu au kikamilifu huduma za saratani kwa sababu ya shinikizo linalotokana na ugonjwa wa COVID-19 kwa mifumo ya afya na vizuizi vya usafiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.