Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Coronavirus: Zaidi ya kesi 20,300 na vifo zaidi ya 1,000 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya virusi vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 2,088,400, baada ya visa vipya 20,398 kuripotiwa siku iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza nchini Ujerumani ya Robert Koch (RKI).

Makao makuu ya kampuni ya Kijerumani ya biotech firm BioNTech
Makao makuu ya kampuni ya Kijerumani ya biotech firm BioNTech REUTERS/Kai Pfaffenbach/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia inaripoti vifo vipya 1,013, na kufikisha jumla ya vifo 49,783 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

 

Maafisa wameonya kuwa ipo haja ya juhudi mpya kuwekwa ili kudhibiti kasi ya maambukizo kufuatia ongezeko la watu kuambukizwa virusi vya Corona katika siku za hivi karibuni.

 

Hivi karibuni shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya viongozi wa dunia kuwa makini na aina mpya ya kirusi ya kirusi cha Corona..

Idadi ya nchi zinazokabiliwa na aina mpya ya kirusi cha Corona kilichoanzia nchini Uingereza imefikia hamsini na nchi 20 zinakabiliwa na kirusi cha aina hiyo kilichoanzia nchini Afrika Kusini, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aina ya tatu ya kirusi cha Corona ambacho Japani ilitangaza Jumapili Januari 10 inaweza kuathiri jibu la kinga na kuna haja ya kuitathimini zaidi, kulingana na WHO, ambayo inabaini katika jarida lake la kila wiki "aina mpya ya Corona inayotia wasiwasi".

"Kadiri virusi vya SARS-CoV-2 vinavyoenea, athari inaendelea kuwa kubwa zaidi katika nchini mbalimbali duniani," inasema WHO.

"Viwango vya juu vya maambukizi vinamaanisha kwamba watu wanapaswa kutarajia hali mbaya zaidi kuibuka."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.