Pata taarifa kuu
BARA ULAYA

COVID-19: Chanjo ya Moderna kutumiwa barani Ulaya

Shirika la madawa la Umoja wa Ulaya (EMA) limeidhinisha chanjo nyingine dhidi ya COVID-19 ya Moderna inayotengenezwa na maabara ya Marekani, ikiwa ni chanjo ya pili ambayo inaidhinishwa kutumiwa katika Umoja wa Ulaya.

Chanjo aina ya Moderna
Chanjo aina ya Moderna Photo AP / Hans Pennink
Matangazo ya kibiashara

"EMA imeagiza kuuzwa kwa masharti chanjo ya Moderna dhidi ya COVID-19 kwa kuzuia magonjwa kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18", kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka ya Ulaya ya Udhibiti wa Dawa, yenye makao yake makuu huko Amsterdam.

Idadi ya maambukizi imeongezeka barani Ulaya.  Wananchi wengi wa bara la Ulaya wanalalamika juu ya kasi ndogo ya utoaji wa chanjo ya awali ya Pfizer na BioNTech.

Nchi nyingi za Ulaya zinaendelea kukumbwa na aina mpya ya virusi vya Corona, iliyoanzia nchini Uingereza. Aina hii mpya ya Corona inasambaa kwa kasi kulingana na vyanzo kutoka shirika la Afya Duniani, WHO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.