Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Covid 19: Idadi ya vifo yaongezeka hadi zaidi ya vifo 35,000 Ujerumani

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,787,410, baada ya visa vipya 11,897 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwilu zilizotolewa na taasisi ya Ujerumani ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Robert Koch (RKI).

Mhudumu wa afya akiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa
Mhudumu wa afya akiendelea na kazi ya kutoa huduma kwa mgonjwa REUTERS/Kacper Pempel
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vya vipya 944, na na kusababisha jumla ya vifo 35,518 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Kutokana na hali ya kuongezeka kwa vifo na maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani, inaelekea kutakuwapo na makubaliano kwenye majimbo yote 16 juu ya kurefusha muda wa kutekeleza hatua kali za kuzuia kuenea kwa maambukizi.

Muda wa hapo awali ulikuwa hadi tarahe 10 mwezi huu. Uamuzi utatolewa Jumanne kwenye mkutano kati ya mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Mlipuko wa virusi vya Corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.