Pata taarifa kuu
UJERUMANI-COVID 19-AFYA

Covid 19: Karibu visa vipya 11,000 vyaripotiwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,651,834, baada ya visa vipya 10,976 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumatatu na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Kirusi cha  corona
Kirusi cha corona Radoslav Zilinsky/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 348, na kufikisha jumla ya vifo 30,126 tangu kuanza kwa janga hilo nchini.

Hayo yanajiri wakati zoezi la utoaji chanjo dhidi ya virusi vya Corona lilianza rasmi Jumamosi katika majimbo 16 ya Ujerumani. Watu wa kwanza kupatiwa chanjo walikuwa ni wale walio na umri wa zaidi ya miaka 80, wauguzi na wafanyakazi wa hospitali ambao wako katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi hivyo.

Serikali imewahimiza wananchi kupewa chanjo kwa manufaa yao na kuwalinda wengine. Wataalamu wamesema kiwango cha asilimia 60 hadi 70 cha chanjo ni muhimu ili kuweza kudhibiti kirusi hicho.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani, WHO, lilionya kwamba janga hilo la sasa halitakuwa la mwisho na kwamba ni muda wa kujifunza kutoka janga la virusi vya Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.