Kesi ya kwanza ya aina mpya ya Corona chathibitishwa Ufaransa
Ufaransa imerekodi kesi ya kwanza ya aina mpya ya virusi vya Corona iliyoanzia nchini Uingereza. Mtu huyo aliyeabukizwa kirusi hicho alipatikana huko Tour, Wizara ya Afya imetangaza siku ya Ijumaa usiku.
Imechapishwa:
Mtu aliyeambukizwa ni raia wa Ufaransa anayeishi nchini Uingereza. ameonekana na dalili za aina hiyo mpya ya Ugonjwa aw COVID-19 na amewekwa karantini nyumbani kwake, imesema taarifa.
Mfaransa huyo aliyewasili "kutoka London mnamo Desemba 19", "anapewa matibabu katika hopitali ya CHU tangu Desemba 21 baada ya kupatikana na maambukizi ya virusi hivyo", imesema Wizara ya Afya, ambayo imehakikisha kwamba ni "kisa cha kwanza cha maambukizi ya aina mpya ya virusi vya Corona ” ambacho kimegunduliwa nchini Ufaransa.
"Mamlaka ya afya inaendelea kutafuta wahudumu wa afya ambao walikuwa wakimhudumia mgonjwa huyo na watu waliotangamana naye, ili waweze kuwekwa karantini, ili kudhibiti kuenea kwa aina hiyo pya ya virusi vya Corona, ambavyo ni hatari binadamu", kimesema kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa nchini Ufaransa.
Kisa kama hicho kimeripotiwa nchini Ujerumani, ambaye ni mwanamke aliyewasili kwa ndege kutoka London, na pia nchini Lebanoni kisa kingine kimethibitishwa kwa abiria aliyetokea London, nchini Uingereza.
Mataifa ya Uhispania, Italia na Uholanzi pia yametangaza visa hivyo.