Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Coronavirus: Zaidi ya vifo 900 vyathibitishwa nchini Ujerumani

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,379,238, baada ya visa vipya 27,728 kuthibitishwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimi zilizotolewa leo Jumatano na kiyuo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel REUTERS/Annegret Hilse/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hiyo pia imeripoti vifo vipya 952, na kufikisha jumla ya vifo 23,427 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Biashara zote ambazo sio muhimu, pamoja na shule na vitalu vimefungwa nchini Ujerumani kuanzia leo Jumatano Desemba 16 hadi Januari 10, 2021, Kansela Angela Merkel alitangaza Jumapili, katika jaribio la kuzuia mlipuko wa pili wa virusi vya Corona.

Baada ya kubainika 'vifo vingi' kutokana na janga la COVID-19 na "kuongezeka kwa visa vingi" vya maambukizi, kiongozi huyo wa kihafidhina, aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP, alisema: "tunalazimika kuchukua hatua na tunaanza kuzitekeleza sasa."

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.