Pata taarifa kuu
COVID 19-UJERUMANI

Coronavirus: Idadi ya vifo nchini Ujerumani yapindukia zaidi ya 20,000

Idadi ya visa vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Ujerumani imepanda hadi 1,242,203, baada ya visa vipya 23,679 kuripotiwa siku moja iliyopita, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Alhamisi na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI).

Upimaji wa maambukizi ya Corona nchini Ujerumani
Upimaji wa maambukizi ya Corona nchini Ujerumani REUTERS/Alexandre Meneghini
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Robert Koch (RKI) pia kinaripoti vifo vipya 440, na kufikisha jumla ya vifo 20,372 tangu kuzuka kwa janga hilo nchini Ujerumani.

Ujerumani ni mojawapo ya nchi za Ulaya ambazo zimeendelea kurekodi idadi kubwa ya visa vipya vya maambukizi.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.