Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-BIASHARA

Boris Johnson: Kuna uwezekano wa kufikia mkataba wa kibiashara na Umoja wa Ulaya Jumapili

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, amesema bado kuna uwezekano wa kufikia mkataba wa kibiashara hadi hapo siku ya Jumapili wiki hii baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Johnson ameyasema hayo Jumatano wiki hii akiwa nchini Uingereza kabla ya kuanza safari yake kuelekea Brussels Ubelgiji, kwa mazungumzo na rais wa tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Ameliambia bunge kuwa bado kunapaswa kuwa na makubaliano mazuri.

Katika mazungumzo yake na na von der Leyen kuhusu suala hilo usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Johnson amefahamisha kuwa wamekubaliana kuwa huenda muafaka ukapatikana hadi kufikia siku ya Jumapili wiki hii.

Katika tukio jingine mapema jana, kansela wa Ujerumani Angela Merkel pia alisema bado anaona kuna nafasi ya makubaliano baada ya Uingereza kuondoka kikamilifu katika umoja huo.

Lakini ameonya kwamba Umoja wa Ulaya utapinga kile alichokitaja kuwa masharti yasiyokubalika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.