Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA-USHIRIKIANO

Zaidi ya dola milioni 500 kutolewa dhidi ya COVID-19 katika mkutano wa amani wa Paris

Nchi na mashirika ya kibinafsi yanayounga mkono juhudi za Shirika la Afya Duniani, WHO, kupambana na COVID-19 yanatarajia leo Alhamisi kuahidi kutoa zaidi ya dola milioni 500 (Euro milioni 425) kwa jumla kuunga mkono mpango huo.

Mpango wa ACT-Accelerator ulizinduliwa mnamo mwezi Aprili na shirika la Afya Duniani, WHO.
Mpango wa ACT-Accelerator ulizinduliwa mnamo mwezi Aprili na shirika la Afya Duniani, WHO. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ahadi hizi zitatolewa katika mkutano wa Amani wa Paris, hafla ya kila mwaka iliyozinduliwa mnamo mwaka 2018 na rais Emmanuel Macron, waandaaji wa mkutano huo wamesema.

Ufaransa itaahidi kutoa euro milioni 100 na Uhispania euro milioni 50. Uingereza itaahidi kutoa pauni moja kwa dola nne zilizotangazwa.

Wakfu wa Bill na Melinda Gates kwa upande wake utatangaza "mchango mkubwa", kulingana na waandaaji wa mkutano.

Mpango wa ACT-Accelerator ulizinduliwa mnamo mwezi Aprili na shirika la Afya Duniani, WHO. Huu ni mradi wa ushirikiano wa kimataifa kuharakisha maendeleo, uzalishaji na kupata kiwango sawa katika masuala ya vipimo, tiba na chanjo dhidi ya COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.