Pata taarifa kuu
ULAYA-CORONA-AFYA

Nchi za Ulaya zajaribu kuchukuwa hatua kali dhidi ya Corona

Mataifa ya Ulaya yameendelea kuweka masharti makali zaidi ya kujikinga kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona, ugonjwa ambao umeambukiza watu zaidi ya milioni 18 na kuwauwa wengine karibu laki saba.

Uvaaji barakoa ni lazima katika jiji lote la Laval tangu Jumatatu Agosti 3, 2020.
Uvaaji barakoa ni lazima katika jiji lote la Laval tangu Jumatatu Agosti 3, 2020. RFI / Stéphane Geneste
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa na Uholanzi zimefanya uvaaji barakoa kuwa lazima, huku Uingereza ikichelewesha kurejesha shughuli za kawaida.

Wakati huo huo China na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinajadili mipango ya kubaini chanzo cha mripuko wa virusi vya corona, kufuatia ziara nchini humo, ya wataalamu wawili wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa.

Virusi vya Corona vilibainika kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan katikati mwa China, mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, na vimehusishwa na soko la jumla la vyakula, ambako wanyama wa porini wanauzwa.

Hivi karibuni Shirika la Afya Duniani lilionya kuwa ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona miongoni mwa vijana barani Ulaya, ni tishio kubwa la kuongezeka kwa maambukizi hayo katika bara hilo.

Mwakilishi wa WHO barani Ulaya Hans Kluge, alisema ongezeko la hivi karibuni limeonakana kwa vijana na viongozi wa mataifa mbalimbali wana jukumu la kuwasiliana ipasavyo  na vijana na kuwafikishia ujumbe kuhusu maambukizi ya Corona.

Aidha, alisema ongezeko hili linatokana na vijana wengi barani Ulaya ambao wameshindwa kubadilisha tabia zao hata baada ya kuzuka kwa janga hili.

Ripoti zinasema kuwa vijana wengi wameendelea kukaidi ushauri wa kutokusanyana na kufanya sherehe au kwenda katika maeneo ya kitalii ili kuepuka maambukizi hayo.

Hivi karibuni, serikali ya Uingereza iliwamiliza wananchi wa taifa hilo, hasa vijana kupunguza uzito kwa kubadilisha mfumo wao wa kula ili kusaidia katika mapambo dhidi ya janga hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.