Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA-USHIRIKIANO

Brexit: Mazungumzo kati ya EU na London kuanza

Mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza kujaribu kupata makubaliano ya biashara ya baada ya nchi hiyo kujitoa katika umoja huo yanatarajiwa kuanza tena Jumatatu hii Juni 1.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Mei 28, 2020, Februari 12, 2020.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Mei 28, 2020, Februari 12, 2020. REUTERS/Hannah McKay
Matangazo ya kibiashara

Boris Johnson ametangaza kuwa atashiriki katika mazungumzo hayo kujaribu kupata mkataba wa kibiashara na Brussels, kiongozi wa ujumbe katika mazungumzo hayo kwa upande wa Uingereza, David Frost, aliwaambia wabunge wa Uingereza Jumatano wiki iliyopita.

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya baada ya Brexit Michel Barnier ameitahadharisha Uingereza kuwa iwapo haitozingatia azimio la kisiasa lilioidhinishwa na pande mbili msimu wa mapukutiko mwaka uliopita, hakutakuwa na mkataba baina yao unaoweza kufikiwa.

"The clock is ticking", "muda unakwenda", maneno haya matatu kwa Kiingereza, Michel Barnier alikuwa akiyasema mara kwa mara mwaka jana.

Barnier ameituhumu Uingereza kwa kutotimiza ahadi zake na kuonya hakutakuwa na makubaliano ikiwa haitabadilika.

"Serikali ya Uingereza imechukua mkondo wa kila wakati kubadili au kupuuza utekelezaji wa ahadi iliyokwishazitoa, " Barnier ameliambia gazeti la Sunday Times.

Umoja wa Ulaya na Uingereza wana hadi mwishoni mwa mwaka huu kukamilisha majadiliano ya kupatikana mkataba wa biashara wa baada ya Brexit.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.