Pata taarifa kuu
POLAND-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa rais kuahirishwa Poland

Itakuwa vigumu kuandaa uchaguzi wa rais nchini Poland katika tarehe iliyopangwa ya Mei 10, Waziri Mkuu wa Poland, Jacek Sasin amesema Jumatatu wiki hii, huku akibaini kwamba kuna uwezekano uchaguzi huo uahirishwe Mei 17 au Mei 23.

Polond imepanga uchaguzi wa urais kufanyika Mei 10 wakati nchi hii inakabiliwa na janga la Covid-19.
Polond imepanga uchaguzi wa urais kufanyika Mei 10 wakati nchi hii inakabiliwa na janga la Covid-19. Wojtek RADWANSKI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Chama tawala cha Haki na Sheria cha PiS, kinajaribu kufanya kilio chini ya uwezo wake ili uchaguzi huo ufanyike licha ya mgogoro wa kiafya uliyosababishwa na virusi vya Corona kwa kupendekeza marekebisho ya sheria za uchaguzi ambao utawezesha upigaji kura unafanyika kupitia njia ya posta.

Lakini sheria inayoruhusu kura hii ya posta bado haijakubaliwa na Bingela Seneti na uchaguzi wa awali unaonyesha kwamba chini ya 30% ya raia wa Poland wako tayari kupiga kura ikiwa uchaguzi utafanyika Mei 10 kama ilivyopangwa.

"Mei 10 itakuwa vigumu," amesema Jacek Sasin kwenye redio binafsi ya Zet. "Ikiwa imesalia wiki moja kabla ya uchaguzi, Braia wa Poland bado hawajui kama watapiga kura. Upinzani na Bunge la Seneti ndio wanahusika na hali hii."

Upinzani nchini poland, makundi ya haki za binadamu na Umoja wa Ulaya wamebaini kwamba kufanyika kwa uchaguzi katika mazingira yaliyowekwa na serikali hakutakuwa na uwazi na kutadhoofisha demokrasia nchini Poland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.