Pata taarifa kuu
UINGEREZA-JOHNSON-CORONA-AFYA

Johnson azuiliwa hospitalini 'kwa hatua za tahadhari'

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, aliyeambukizwa virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19, anaendelea kulazwa hospitalini siku moja baada ya kupokelewa katika hospitali moja ya jijini London ambapo anaendelea kufanyiwa vipimo, shirika la habari la Reuters lililonukuu chanzo cha serikali, limesema.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aendelea kufanyiwa vipimo, baada ya kupatikana na virusi vya Corona..
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aendelea kufanyiwa vipimo, baada ya kupatikana na virusi vya Corona.. REUTERS/Lisi Niesner
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na chanzo hiki, Boris Johnson anaendelea na mamlaka yake kama waziri mkuu, siku kumi baada ya kupatikana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

"Waziri mkuu bado yuko hospitalini. Alilala hospitalini usiku wa kiamkia leo," shirika la habari la Reuters limenukuu chanzo chake.

Boris Johnson ambaye alitakiwa kubaki nyumbani baada ya kupatikana na virusi vya Corona, alipelekwa hospitali Jumapili na daktari wake aliamua kwamba anapaswa kufanyiwa vipimo vipya.

"Kwa ushauri wa daktari wake, Waziri Mkuu alilazwa hospitalini Jumapili jioni kwa vipimo zaidi," ofisi yake (Downing Street) imesema katika taarifa.

"Hii ni hatua ya tahadhari, Waziri Mkuu anaendelea kuwa na dalili za ugonjwa huo siku kumi baada ya kupimwa", Downing Street imeongeza.

Boris Johnson, 55, ambaye alichukuwa madaraka ya uongozi wa nchi hiyo kubwa kiuchumi alikuwa kiongozi wa kwanza kutangaza kuwa amepatikana na virusi vya Corona Machi 27.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Rais wa Marekani Donald Trump alituma ujumbe wa kuonesha uungwaji wake mkono kwa Boris Johnson.

"Wamarekani wote wanamuombea3, amesema rais Donald Trump. "Ni rafiki, muungwana na kiongozi mkubwa na kama mnavyojua, alilazwa hospitalini Jumapili jioni lakini natumai na nina uhakika kuwa atapona."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.