Pata taarifa kuu
UINGEREZ-EU-UCHAGUZI

Hatma ya Uingereza kujulikana baada ya uchaguzi

Wananchi wa Uingereza hivi leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa tatu kufanyika chini ya miaka mitano, uchaguzi ambao unatajwa kuwa ndio utakaotoa hatma ya nchi hiyo kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Mmoja wa waandamanaji wanaopinga Uingerza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya akishikilia bendera ya Umoja wa Ulaya mbele ya makao makuu ya Bunge hukoLondon, Uingereza, Oktoba 25, 2019.
Mmoja wa waandamanaji wanaopinga Uingerza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya akishikilia bendera ya Umoja wa Ulaya mbele ya makao makuu ya Bunge hukoLondon, Uingereza, Oktoba 25, 2019. REUTERS/Henry Nicholls
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafuatia ule wa mwaka 2015 na 2017, ambapo uchaguzi wa safari hii unatajwa kuwa wa ushindani ukilinganisha na ule uliyopita, kutokana na hofu kuwa vyama vidogo huenda vikafanya maajabu.

Uchunguzi wa maoni ya wapiga kura umetabiri kwamba matokeo ya uchaguzi yatakaribiana katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wenye lengo la kutatua mzozo wa Brexit.

Bunge la Uingereza mara kadhaa lilikataa kukubali masharti ya kuachana na Umoja wa Ulaya ambapo waziri mkuu wa zamani theresa May alikubaliana na Umoja huo, na kumlazimisha kuacha madaraka na kumuingiza Johnson katika mzozo huo akiahidi kuupatia ufumbuzi. Boris Johnson aliahidi kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya ifikapo Januari 31.

Mchuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya waziri mkuu Boris Johnson na mpinzani wake Jeremy Corbyn ambao kila mmoja amejinasibu kukamilisha mchakato wa Brexit.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.