Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-UFARANSA-USHIRIKIANO

Macron aunga mkono mazungumzo zaidi ya mwezi mmoja kutafuta suluhisho la Brexit

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameunga mkono kufanyika kwa mazungumzo zaidi kuhusu nchi ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya lakini, ametupilia mbali uwezekano wa kubadilishwa kwa kipengele kuhusu eneo la mpaka la nchi ya Ireland Kaskazini.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (kushoto) Agosti 22,2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akikutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson (kushoto) Agosti 22,2019. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Uingereza ilijibu kwa kusema haitaweka upekuzi katika mpaka huo, na kuleta uwezekano kwamba Umoja wa Ulaya utalazimika kuamua jinsi ya kushughulikia mpaka huo kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza.

Akiunga mkono kauli ya kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, rais Macron ameunga mkono kuongezwa kwa muda wa mwezi mmoja zaidi wa kufanyika mazungumzo ili kuhakikisha Uingereza haijiondoi bila mkataba.

Kipengele kuhusu kuwa na ukaguzi wa kina kwenye mpaka wa Uingereza na Ireland Kaskazini kimeendelea kuwa kikwazo katika safari ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, taifa hilo likitaka kipengele hicho kiondolewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.