Pata taarifa kuu
UFARANSA-LEBANON

Saad Hariri kukutana na Emmanuel Macron nchini Ufaransa

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Lebanon, Saad Hariri, leo Jumamosi, ameondoka nchini Saudi Arabia kuelekea Ufaransa, kwa lengo la kupunguza magogoro wa kisiasa uliotokana na kujiuzulu kwake kwa ghafla huko Riyadh.

Waziri wa zamani wa Lebanon  Saad Hariri
Waziri wa zamani wa Lebanon Saad Hariri REUTERS/Mohamed Azakir
Matangazo ya kibiashara

Hariri na mke wake watakutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris baada ya tuhuma kutoka kwa wapinzani wa kisiasa wa Hariri nchini Lebanon kwamba anashikiliwa mateka na mamlaka ya Saudi Arabia.

Kuondoka kwa Hariri, mwenye umri wa miaka 47, kumekuja baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian mjini Riyadh siku ya Alhamisi wakati huu Ufaransa ambayo zamani iliifanya Lebanon kuwa koloni lake ikijaribu kupunguza mgogoro ambao umesababisha mvutano kati ya mahasimu wa kikanda Iran na Saudi Arabia.

Katika kuenea zaidi kwa hali hiyo, vyombo vya habari vya serikali ya Saudi Arabia vimesema hii leo Jumamosi kuwa nchi hiyo imemwita nyumbani balozi wake mjini Berlin kama hatua ya kupinga maoni yaliyotolewa na waziri wa kigeni wa Ujerumani, Sigmar Gabriel, yaliyochukuliwa kama yanayoeleza kwamba Hariri anashikiliwa kinyume na hiari yake huko Riyadh.

Hariri alitangaza kujiuzulu wadhifa huo mnamo Novemba 04 mwaka huu na kuzua sintofahamu .

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.