Pata taarifa kuu
LEBANON-UFARANSA-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Hariri kwenda Ufaransa kwa "mwaliko" wa Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemualika Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu Saad Hariri, kwenda Ufaransa kwa siku chache zijazo na familia yake.

Wananchi wengi wa Lebanoni wamekua wakiishtumu Saudi Arabia kumshawishi Saad Hariri kujiuzulu.
Wananchi wengi wa Lebanoni wamekua wakiishtumu Saudi Arabia kumshawishi Saad Hariri kujiuzulu. REUTERS/Jamal Saidi
Matangazo ya kibiashara

Bw. Hariri amekubali mwaliko huo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, ambaye aliwasili mjini Riyadh siku ya Jumatano usiku, alikutana na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambapo alizungumzia kuhusu utaratibu wa kuondoka kwa Saad hariri kwenda Paris.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemualika waziri Saad Hariri na familia yake kwenda lakini amesema kuwa hampi hifadhi ya kisiasa.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu Saad Hariri yuko huru kuondoka Saudi Arabia " kwa wakati wowote" (Adel al-Jubeir)

Maafisa wa Ufaransa wanasema kuwa Bw. Hariri atawasili siku chache zinazokuja.

Serikali ya Saudi Arabia imekana kumzuilia bila ya mapenzi yake au kumlazimisha kujiuzulu katika jitihada za kukabiliana ushawishi wa hasimu wake Iran.

Rais wa Lebanon Michel Aoun amekaribisha juhudi za Ufaransa katika kumshawishi Saada Hariri kuondoka nchini Saudi Arabia

Bw. Macron akiongea wakati alifanya ziara nchini Lebanon alisema mwaliko huo wa kuzuru Ufaransa ulitolewa wakati alizungumza na Bw Hariri na mfame wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kwa njia ya simu.

Bw. Hariri alijiuzulu ghafla wakati akiwa ziarani nchini Saudi Arabia tarehe 4 Novemba, na kuzua msuko suko wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.