Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRMA-TABIA NCHI

Macron azuru maeneo yanayomilikia na Ufaransa yaliyokumbwa na kimbunga Irma

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametetea jitihada za serikali yake inavyoshughulikia kimbuga kilichopewa jina la Irma katika visiwa inavyomiliki katika mataifa ya Carribean.

Rais Macron azuru St Martin, Septemba 12, 2017, mbele ya nymba zilizoharibiwa na Kimbunga Irma.
Rais Macron azuru St Martin, Septemba 12, 2017, mbele ya nymba zilizoharibiwa na Kimbunga Irma. REUTERS/Christophe Ena/Pool
Matangazo ya kibiashara

Emmanuel Macron aliwasili muda mfupi kabla ya 10:00 katika kisiwa cha St-Martin, ambapo alikutana na waathirika wa kimbunga Irma, kabla ya kusafiri kwenda St Barthelemy. Kisha alisafiri kwenda St. Martin kabla ya kurudi Guadeloupe Jumatano hii asubuhi.

Rais Macron anatarajia kutembelea waatirika wa kimbunga Irma katika mji wa Guadeloupe na kukutana kwa mazungumzo na viongozi katika mji huo.

"Kurudi kwa hali ya kawaida ni kipaumbele cha juu kwa serikali ya Ufaransa," rais Emmanuel Macron amesema kwenye uwanja wa ndege wa Pointe-à-Pitre. "St-Martin itakarabatiwa upya, ninajikubalisha hilo," amesema.

Akiongozana na mawaziri wa Outre-mer, wa Elimu na Afya,a lisema idadi ya watu waliopoteza maisha ni 11 na "wengi walijeruhiwa na wengine walitoweka" baada kimbunga Irma kuyakumba maeneo haya.

Macron amesema serikali yake imekuwa ikiwasaidia watu walioathirika na kimbuga hicho pindi tu iliposikia kuzuka kwa janga hilo ikiwa ni pamoja na kutuma wanajeshi wake karibu elfu mbili kuwasaidia watu.

Kimbunga hicho kimesababisha vifo vya watu 11 katika kisiwa cha West Indies huku mali za watu zikiharibika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.