Pata taarifa kuu
UFARANSA-SHERIA ZA KAZI

Muswada wa sheria za kazi kuwasili Bungeni Jumanne hii

Rasimu ya sheria za kazi inayoendelea kuibua hali ya sintofahamu nchini Ufaransa inatazamiwa kuwasilishwa Bungeni Jumanne hii na itajadiliwa kwa muda wa wiki mbili chini ya shinikizo kutoka mitaani. Hayo yanajiri wakati ambapo kuna tishio linalolazimisha muswada huo wa sheria upitishwe.

Waziri wa Kazi Myriam El Khomri wakati alipokua akihojiwa maswali bungeni Aprili 5, 2016 mjini Paris.
Waziri wa Kazi Myriam El Khomri wakati alipokua akihojiwa maswali bungeni Aprili 5, 2016 mjini Paris. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mijadala ya Bunge itafunguliwa Jumanne hii mchana na Waziri wa Kazi Myriam El Khomri, ambaye amesema "wakati wa Bunge umewadia" baada ya siku nne ya uhamasishaji wa kitaifa na Mei 1 dhidi ya rasimu ya sheria za kazi, bila kuhesabu maandamano yaliyokua yakifanyika usiku katika miji kadhaa kwa kipindi cha mwezi mzima.

Lakini tangu asubuhi, muungano wa vyama vya wafanyakazi vinaotaka mageuzi CFE-CGC, kwa upande mmoja, na vyama vya wafanyakazi vinavyopinga rasimu hiyo mpya (CGT, FO, FSU na Solidaires), vikiambatana na wawakilishi wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu na shule za sekondari, kwa upande mwingine, wamepanga kukusanyika karibu na majengo ya Bunge (Palais Bourbon).

Hali hii inatokea wakati ambapo Mei 3 ni siku ambayo chama cha FO (FRONT POPULAIRE) kinaadhimisha miaka 80 ya uhai wake. Kiongozi wa FO, Jean-Claude Mailly, amemtolea wito François Hollande na Manuel Valls wa "kutosaliti" moja ya nguzo za sera za chama hicho, akiwaomba "kuweka mbele mazungumzo."

Mpaka sasa kura 40 bado zinakosa ili idadi ya wabunge inayohitajika iweze kupitisha muswada huu wa sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.