Pata taarifa kuu
EU-WAHAMIAJI-USALAMA

EU yazitaka nchi wanachama kugawana wahamiaji

Rais wa Tume ya Ulaya amewasilisha Jumatano wiki hii maelezo ya mpango wa Ulaya yanayopanga mapokezi kwa wakimbizi 160,000 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Jean-Claude Juncker (kushoto), Rais wa Tume ya Ulaya, na Martin Schulz, Rais wa Bunge la Ulaya, Septemba 9, mjini Strasbourg.
Jean-Claude Juncker (kushoto), Rais wa Tume ya Ulaya, na Martin Schulz, Rais wa Bunge la Ulaya, Septemba 9, mjini Strasbourg. Jean-Claude Juncker (g.), président de la Commssion européenne,
Matangazo ya kibiashara

Jean-Claude Juncker ametolea wito nchi wanachama kukubali kuanzishwa kwa "utaratibu wa kudumu " wa idadi maalum, kanuni ambayo imekutana na upinzani mkubwa, hasa mashariki mwa Ulaya.

Suala la uhamiaji limekuwa kwenye ajenda ya hotuba ya kwanza ya Jean-Claude Juncker mbele ya Bunge la Ulaya mjini Strasbourg.

Rais wa Tume ya Ulaya amethibitisha nia yake ya kuweka mpango barani Ulaya unaopanga mapokezi kwa wakimbizi 160,000, katika kipindi cha miaka miwili ijayo. Jean-Claude Juncker pia ametoa wito kwa mara nyingine wa kuweka idadi maalum, ili kuruhusu zoezi la kuwagawana wakimbizi kati ya nchi hizo ishirini na nane wanachama wa Umoja wa Ulaya.

"Sio wakati wa kuwa na hofu"

" Ni wakati wa kuchukua hatua ya ujasiri, yenye uamzi na ya pamoja ya Umoja wa Ulaya, ya taasisi zake na ya wanachama wake wote. Kwanza ni suala la ubinadamu na lenye heshima ya ubinadamu. Kwa upande wa Ulaya, pia ni suala la haki katika mwanga wa historia ", Juncker amewambia wabunge wa Umoja wa Ulaya. " Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, karibu watu 500 000 wameingia Ulaya, lakini huu sio wakati wa kuwa na hofu ", ameongeza Juncker.

Siku chache kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya juu ya suala la sera za uhamiaji, utakaofanyika Septemba 14 mjini Brussels, nchini Ubelgiji, Jean-Claude Juncker amewahimiza "kufikia makubaliano" katika kanuni ya "kuwapatishia hifadhi kwa dharura wakimbizi 160,000" waliopo kwa sasa nchini Ugiriki, Italia na Hungary, kwa misingi ya kugawana idadi sawa.

Tayari Umoja huo ulikuwa umekubaliana kugawana wahamiaji elfu 40 hapo awali kabla ya idadi kuongezeka na kufikia 120,000.

Haijafahamika hata hivyo ni wakimbizi wangapi watakaogawanywa katika nchi hizo.

Tume hiyo pia imezitaka nchi za Ulaya kuwaruhusu wakimbizi hao kuanza kufanya kazi wanapowasili katika nchi hizo ili kujipatia kipato.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.