Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALAYSIA-UCHUNGUZI

Bawa lililopatikana ni la ndege MH370

Bawa la ndege lililopatikana wiki iliyopita katika Bahari ya Hindi ni la MH370, ndege ya shirika la Malaysia Airlines, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014, Waziri mkuu wa Malaysia ametangaza Alhamisi wiki hii.

Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak, katika mji wa Kuala Lumpur, Agosti 5, mwaka 2015.
Waziri mkuu wa Malaysia, Najib Razak, katika mji wa Kuala Lumpur, Agosti 5, mwaka 2015. REUTERS/Olivia Harri
Matangazo ya kibiashara

Saa chache za uchunguzi zimetosha kwa wataalam waliokusanyika katika maabara ya kijeshi karibu na mji wa Toulouse kuthibitisha kile watu wengi walikua wakisubiria: Bawa hilo lilisukumwa na mawimbi ya bahari Hindi kutoka kilomita kadhaa ya eneo ndege ilipoangukia, hadi nchi kavu, Najib Razak amesema wakati wa mkutano ulioandaliwa katikati ya usiku katika mji wa Kuala Lumpur.

" Leo hii, siku 515 baada ya ndege hiyo kutoweka, ni kwa moyo mzito ninawatangazieni kwamba timu ya wataalam wa kimataifa imehitimisha kuwa bawa lililopatikana katika kisiwa cha Réunion ni la MH370, ndege ya Malaysia Airlines iliotoweka mwaka jana MH370 ", ameongeza Waziri mkuu wa Malaysia.

Watu wengi walikua na mashaka ya eneo bawa hilo lilikotokea wakati viongozi wa Malaysia walithibitisha tangu Jumapili Agosti 2 kwamba si bawa la ndege hiyo iliyotoweka mwaka mmoja uliopita bali ni bwawa la ndege aina ya Boeing 777. Lakini tangu uzinduzi wa mtindo wa ndege hizi mwaka 1995, ndege mbili pekee aina ya Boeing 777 zilifanya ajali na kuwaua watu wengi. Ajali hizi zilitokea katika bahari Hindi. Lakini ilibidi kuwepo na uhakika.

Ni jukumu la utaalamu lililoanza Jumatano mchana katika maabara ya kijeshi katika mji wa Balma, karibu na mji wa Toulouse. Wameshiriki katika zoezi hilo wataalam wa Ofisi ya Upelelezi na uchambuzi (BEA) kutoka Ufaransa na wenzao wa Malaysia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.