Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki yapewa muda wa mwisho kuhusu mpango mpya

Mataifa ya Umoja wa Ulaya yanayotumia sarafu ya Euro yameipa serikali ya Ugiriki hadi kesho Alhamisi kuja na mapendekezo mapya ya kuafikiana na wakopeshaji wa Kimataifa kuhusu deni linaloikabili nchi hiyo ya Ugiriki.

Martin Schulz (kushoto), rais wa Bunge la Ulaya, Alexis Tsipras (kulia), waziri mkuu wa Ugiriki ambaye leo Jumatano asubuhi anatazamia kujieleza mbele ya Bunge la Ulaya.
Martin Schulz (kushoto), rais wa Bunge la Ulaya, Alexis Tsipras (kulia), waziri mkuu wa Ugiriki ambaye leo Jumatano asubuhi anatazamia kujieleza mbele ya Bunge la Ulaya. REUTERS/Marko Djurica
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza la Umoja huo Donald Tusk amesema huu ni wakati muhimu kwa Ugiriki na nchi zinazotumia sarafu ya Euro kupata mwafaka.

Hatua hii inakuja wakati huu, viongozi wa Umoja wa Ulaya wakaitarajiwa kukutana siku ya Jumapili jijini Brussels kujadili hali ya kiuchumi ya Ugiriki.

Rais wa Ufaransa François Hollande amesema tatizo hili si tu la Ugiriki bali ni la Umoja wa Ulaya kuelekea miaka ijayo.

Siku moja baada ya kura ya maoni nchini Ugiriki na raia kupiga kura ya "hapana" dhidi ya masharti yaliyowasilishwa na wakopeshaji wa nchi hiyo, rais wa Ufaransa François Hollande alimpokea Jumatatu jioni wiki hii Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ili kuonesha umoja wao juu ya Ugiriki.

Angela Merkel na François Hollande walizungumza kwa muda wa saa moja na nusu. Kufuatia mkutano wao huo, marais hao wawili walitoa tangazo la pamoja fupi, ambapo wamemfahamisha Alexis Tsipras kwamba " mlango bado uko wazi " licha ya ushindi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wakopeshaji wa Ugiriki.

Lakini kwa kurudi kwenye meza ya mazungumzo, rais wa Ufaransa na Kansela wa Ujerumani wamemuomba waziri mkuu wa Ugiriki kufanya mapendekezo ya kweli na yenye kuaminika ili kuweka mpango huo katika muda muafaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.