Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MAANDAMANO-UHAMIAJI-UISLAM-HAKI-USALAMA

Maandamano yaitikisa miji ya Ujerumani

Nchi ya Ujerumani imeshuhudia maandamano makubwa zaidi kuwahi kufanyika nchini humo ya watu wanaopinga sera ya uhamiaji pamoja na kile wanachodai ni kuenezwa kwa uislamu barani Ulaya. 

Wafuasi wa kundi linalopiga vita Uislam (Pegida) wameandamana katika mji wa Dresd Januari 5 mwaka 2015.
Wafuasi wa kundi linalopiga vita Uislam (Pegida) wameandamana katika mji wa Dresd Januari 5 mwaka 2015. REUTERS/Fabrizio Benscha
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya waandamanaji elfu 18 walijitokeza kwenye miji mbalimbali nchini humo wakikaidi wito uliotolewa na kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ambaye aliyataka makundi hayo kutojihusisha na aina hii ya maandamano.

Kundi la PEGID kutoka mrengo wa kulia na limejipambanua kwa sera zake za kupinga sera za uhamiaji na uenezwaji wa Uislam barani Ulaya, liliitisha maandamano katika mji wa Dresden ambao unakaliwa na wageni wengi kutoka baadhi ya mataifa ya Uarabuni.

Katika maandamano hayo pia yalifanyika maandamano ya makundi mengine ambayo yanalipinga kundi hili kwa kile wanachodai halina lengo jema wakati huu dunia ikiishi kama kijiji kimoja.

Maandamano kama haya yalifanyika kabla ya sherehe za Krismasi mwaka uliopita kwenye miji ya Berlin, Stuttgart na Cologne, maandamano ambayo yalipingwa vikali na viongozi wa makanisa, wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.