Pata taarifa kuu
MAREKANI-UFARANSA-URUSI-CHINA-UJERUMANI-UINGEREZA-IRAN-NYUKLIA-DIPLOMASIA

Mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran wafikia kikomo

Viongozi kutoka nchi sita (Ufaransa, Marekani, Urusi, Uingereza, China na Ujerumani) wanakutana mjini Vienna, Austria na viongozi wa Iran ili kutafutia suluhu suala la mpango wa nyuklia wa Iran.

Kusoto-kulia, Laurent Fabius, John Kerry, Catherine Ashton, Philip Hammond na Frank-Walter Steinmeier mjini Vienna, Novemba 23 mwaka 2014.
Kusoto-kulia, Laurent Fabius, John Kerry, Catherine Ashton, Philip Hammond na Frank-Walter Steinmeier mjini Vienna, Novemba 23 mwaka 2014. REUTERS/Joe Klamar/Pool
Matangazo ya kibiashara

Wakati muda wa mwisho wa mazungumzo uliowekwa na mataifa ya magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran ukifikia kikomo leo Jumatatu Novemba 24, wawakilishi wa Marekani na Uingereza wanasema kuwa bado safari ni ndefu na kwamba huenda wasifikie muafaka leo Jumatatu kama walivyopanga.

Mazungumzo haya yamekuwa yakiendelea kufanyika kwa miezi kadhaa hivi sasa huku kukiwa hakuna dalili chanya kuwa Iran itafikia muafaka na nchi za magharibi na hatimaye kumaliza mzozo uliodumu kwa miaka 12 hivi sasa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Akizungumza kwenye mahojiano maalumu na kituo cha CBC cha nchini Marekani, rais Barack Obama amesisitiza umuhimu wa Iran kukubaliana na matakwa ya nchi za magharibi ili kuondolewa vikwazo.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza, Philip Hammond amesema kuwa bado pande hizo ziko mbali sana katika kufikia muafaka na kwamba hili ni tatizo, na kuna uwezekano mkubwa wa kuongezwa kwa muda zaidi.

Jumatatu Novemba 24 siku ya mwisho wa muda uliotengwa na nchi za magharibi kwa nchi ya Iran kukubaliana na masharti iliyowekewa kuhusu mpango wake wa nyuklia ili iondolewe vikwazo, mazungumzo ambayo mpaka kufikia jioni huenda ikajulikana iwapo kuna muafaka umefikiwa au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.