Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-JIHADI-SHERIA

Mwanajihadi kutoka Ufaransa ahukumiwa miaka 8 jela

Kifungo cha miaka minane jela kilitolewa Jumatano Novemba 12 dhidi ya raia wa Ufaransa aliye jiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam nchini Mali.

Jeshi la Mali likipiga doria katika jimbo la Kidal, Mwezi Julai mwaka 2013.
Jeshi la Mali likipiga doria katika jimbo la Kidal, Mwezi Julai mwaka 2013. AFP PHOTO / KENZO TRIBOUILLARD
Matangazo ya kibiashara

Djamel Benhamdi, mwenye umri wa miaka 38, alikamatwa mwezi machi mwaka 2013 nchini Mali. Hukumu dhidi yake imetolewa na Mahakama ya Paris, nchini Ufaransa.

Kifungo hicho kilikua kimeombwa na Mwendesha mashtaka, wakati ambapo majaji hawakuzingatia maelezo ya mtuhumiwa huyo.

Katika utetezi wake, Djamel Benhamdi amesema alikua alitekwa nyara na makundi ya wapiganaji wa kiislam na kulazimishwa kushika silaha.

Djamel Benhamdi amebaini kwamba halijielekeza Mali kujiunga na makundi ya wapiganaji wa kiislam, bali alienda nchini humo kujifunza Qoran. Ni katika hali hiyo aliweza kutekwa nyara, amesema Djamel Benhamdi.

Djamel Benhamdi amejitetea akisema kuwa alisalimu amri mwenyewe wakati alipowaona wanajeshi wa Ufaransa wakipiga doria karibu na pango la jiwe kaskazini mwa Mali mwezi machi mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.