Pata taarifa kuu
MALAYSIA-URUSI-UKRAINE-UHOLANZI-MH17-Uchunguzi-Ripoti-

MH17: ndege ya Malaysia Airlines "ilidunguliwa kwa makombora"

Matokeo ya awali kuhusu ajali ya ndege yenye chapa MH17 ya Malaysia Airlines iliyokua ikitokea Amsterdam, nchini Uholanzi ikielekea Kuala Lumpur nchini Malaysia na kupatwa na ajali katikati ya mwezi wa Julai, yametangazwa jumanne wiki hii.

Maafisa wa idara ya huduma za dharura kutoka Ukraine wakibeba moja ya miili ya watu walikua ndani ya ndege ya Malaysia Airlines, Julai 19 mwaka 2014.
Maafisa wa idara ya huduma za dharura kutoka Ukraine wakibeba moja ya miili ya watu walikua ndani ya ndege ya Malaysia Airlines, Julai 19 mwaka 2014. REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa uchunguzi ambao bado haijakamilika, “ ndege ya Malaysia Airlines ilidunguliwa baadya ya kufyatuliwa makombora mengi yaliyokua yakisafiri kwa mwendo wa kasi”. Uchunguzi huo unaendeshwa na viongozi wa Uholanzi.

Ndege hiyo ya Malaysia Airlines ilichanika vipande ikiwa hewani.” Na hakuna kinachoonesha kuwa ajali ya ndege hiyo ilisababishwa na tatizo la kiufundi au kughafilika kwa marubani”. Matokeo ya awali ya shirika la utafiti la Uholanzi yanaonesha kuwa ndege hiyo ilifyatuliwa makombora ikiwa hewani. Lakini hali hii haifahamiki kwa uhakika kwa wakati huu.

Hakika, wakaguzi hawakuweza kujielekeza kwenye eneo la tukio mashariki mwa Ukraine kutokana na mapigano ambayo yalikua yakiendelea. Katika hatua hii ya uchunguzi, matokeo yametolea kufuatia ushahidi uliyonekana kwenye visanduku vya sauti , na picha au video ziliyorikodiwa angani. Lakini kwa mujibu wa msemaji wa Ofisi ya Upelelezi kwa ajili ya usalama, inawezekana kabisa, bila hata hivo kujielekeza kwenye eneo la tukio, kuthibitisha matokeo tuliyo nayo kwa sasa.

Ni mwezi mmoja na nusu sasa baada ya ndege ya Malasia Airlines iliyokua na abiria 298 kupata ajali hio, huku kiev na mataifa ya magharibi wakiendelea kuwatuhumu waasi wa mashariki mwa Ukraine kuhusika na tukio hilo, wakati ambapo Moscow na waasi hao wakiituhumu Kiev kuwa ndio ilidungua ndege hiyo. Zaidi ya wahanga 200 waliyokua ndani ya ndege hiyo hawajatambulika. Hata hivo uchunguzi unaendelea na ripoti ya mwisho inasubiriwa mwakani katika majira ya joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.