Pata taarifa kuu
IRAQ

Iraq yaomba msaada kwa Marekani

Serikali ya Iraq imeomba rasmi Marekani kutumia ndege zake zisizokuwa na rubani kupambana na wapiganaji wa kiislamu wa ISIL waliochukua miji kadhaa juma hili.Ombi hili la Iraq linakuja muda mfupi tu baada ya wapiganaji hao wa kisunni kuvamia kampuni kubwa ya kusafisha mafuta katika eneo la Baiji kaskazini mwa mji wa Baghdad.

Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki akiwahutubia wananchi kuhusu Usalama wa Taifa, Juni 18 2014
Waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki akiwahutubia wananchi kuhusu Usalama wa Taifa, Juni 18 2014 AFP PHOTO / Ahmed Saad / POOL
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa majeshi ya Marekani Jenerali Martin Dempsey amewaambia maseneta nchini humo kuwa ofisi yake imepokea ombi kutoka kwa serikali ya Iraq ikiitaka Marekani kutumia ndege zake kupambana na wapiganaji hao wanaelekea kuvilemea vikosi vya serikali.

Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al Maliki amekuwa akitoa wito kwa raia nchini humo kuungana kwa kujihami na kuwashambulia wapiganaji toka kundi hili lifahamikalo kama ISIL ambao wanasema lengo lao ni kuichukua serikali.

Wanajeshi wa Iraq kwa sasa wanapambana na wapiganaji hao wa ISIL katika mji wa pili kwa ukubwa wa Mosul kujaribu kuwarudisha nyuma bila mafanikio.

Rais Obama ambaye amekunukuliwa akisema kuwa Marekani haitatuma jeshi kupambana na wapiganaji hao, alikutana na viongozi wa bunge la Congress siku ya Jumatano kujadili mbinu za kuisadia serikali ya Iraq kupambana na wapiganaji hao.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.