Pata taarifa kuu
UKRAINE

Ukraine yakiri kutobabaishwa na hatua ya Urusi kukata usambazaji wa gesi yake

Serikali mpya iliyoko madarakani nchini Ukraine hii leo siku ya jumanne imesema haiwezi kubabaishwa na hatua ya Urusi ambayo hatimaye imekata usambazaji wa gesi nchini Ukraine.Maafisa wakuu wa kampuni ya gesi Gazprom ambayo inayomilikiwa na serikali ya Urusi,  wamesema ni lazima Ukraine ianze kutoa malipo kabla ya kupewa gesi, Hii ikiwa ni Hatua inayochukuliwa baada ya serikali ya Ukraine kuonekana kushindwa kulipa deni kubwa iliyo nayo.

Mabomba ya Gesi nchini Ukraine
Mabomba ya Gesi nchini Ukraine REUTERS/Gleb Garanich/Files
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya kiev imeichukua Hatua hiyo ya urusi kama ni uvamizi mpya dhidi ya Ukraine kwa kile inachokisema kuwa ni kutafuta uungwaji mkono zaidi kutoka kwa watu wa mashariki mwa nchi hiyo, kwa namna ya upekee lakini pia kwa wananchi wote wanaotumia gesi yake.

Kampuni ya serikali ya Ukraine ya Naftogaz chini ya mkuu wake Andriï Kobolev imewahakikishia wananachi zaidi ya milioni 45 kuwa licha ya ukosefu wa gesi kutoka Urusi bado kuna uwezekano wa kuyashawishi mataifa ya ulaya kupeleka kiwango kikubw acha gesi nchini Ukraine.

Wakati uo huo mkuu wa taasisi ya nishati wa umoja wa Ulaya Guenther Oettinger ameonya kuwa nchi wanachama wa umoja huo huenda wakakabiliwa na uhaba wa gesi katika msimu ujao wa baridi kutokana na mzozo huo kati ya Ukraine na Urusi.

Katika Hatua nyingine Madaktari katika Hospitali kuu iliyoko mjini Lougansk nchini Ukraine hii leo siku ya jumanne wamethibitisha kuwa mwanahabari aliyepatwa na risase wakati wa majibizano kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wanaoshirikiana na Urusi mashariki mwa Ukraine.

Kwa mujibu wa duru zilizotolewa na daktari mkuu wa hospitali hiyo Fedir Solianik, Mwanahabari huyo wa kituo cha televisheni ya kitaifa ya Ukraine alifariki wakati wa maandalizi ya kufanyiwa upasuaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.