Pata taarifa kuu
Niger-Ufaransa-Algeria

Kundi la kigaidi la Alqaeda laahidi kutoa video ya mateka

Tawi la Al-Qaeda kaskazini mwa Afrika limearifu kuwa mateka nane kutoka bara la Ulaya ambao wanashikiliwa na kundi hilo wapo hai na kuahidi kuachia video hivi karibuni kuonesha raia watano wa Ufaransa ambao ni miongoni mwa mateka linaowashikilia.

Baadhi ya raia wa Ufaransa wakiandamana kufuatia tukio la kushikiliwa mateka raia wanne wa Ufaransa ambao walitekwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini Niger
Baadhi ya raia wa Ufaransa wakiandamana kufuatia tukio la kushikiliwa mateka raia wanne wa Ufaransa ambao walitekwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda nchini Niger AFP PHOTO JEAN-SEBASTIEN EVRARD
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni maandamano yalifanyika katika maenneo kadhaa ya miji ya ufaransa kupinga utekeji nyara wa wafaransa wanne ambao wamekuwa wakishikiliwa na kundi hilo la kigaidi la Alqaeda kwa takribani siku elfu moja sasa.

Mateka hao ni wafanyakazi wa kampuni ya nyuklia inayomilikiwa na ufaransa sambamba na naibu mkandarasi wa kampuni hiyo walitekwa na kundi la Al Qaeda huko Niger mnamo tarehe 16 mwezi septemba mwaka 2010.

Mateka mmoja aliyejulikana kama Francoise Larribe, ambaye ni mke wa Daniel Daniel ambaye bado anashikiliwa,alikuwa miongoni mwa mateka lakini aliachiwa huru mwaka 2011.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.