Pata taarifa kuu
ITALIA

Papa Francis kuongoza misa yake ya kwanza ya Pasaka

Wakati wakristo duniani kote hii leo wakiadhimisaha sikukuu ya Pasaka,Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anajiandaa kuongoza misa yake ya kwanza ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka huku makumi kwa maelfu ya waumini wa dini hiyo wakitarajiwa kujitokeza katika kanisa la mtakatifu Petro kupata baraka za misa hiyo takatifu katika kalenda ya Kanisa Katoliki. 

Kiongozi mpya wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis
Kiongozi mpya wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis RFI
Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo ya Pasaka itafuatiwa na baraka maalumu itolewayo kwa ajili ya mji wa Roma na dunia nzima ambayo papa ataitoa akiwa katika jengo lilelile ambalo alijitokeza kwa mara ya kwanza mbele ya umma baada ya kuchaguliwa kwake mwezi huu.

Katika mkesha wa Pasaka katika kanisa la mtakatifu Petro jana Jumamosi, papa wa kwanza kutoka nje ya Ulaya kwa karibu miaka 1300 ya historia ya kanisa ,aliwatembelea wapagani na Wakatoliki walioanguka, akiwashawishi kupiga hatua mbele kumuelekea Mungu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.