Pata taarifa kuu
ITALIA

Harakati za uchaguzi mkuu zang'oa nanga nchini Italia

Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti anatarajiwa kutoa uamuzi wake leo jumapili kama atashiriki au hatoshiriki katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwezi february mwakani.

REUTERS/Eric Gaillard
Matangazo ya kibiashara

Monti anatarajiwa kutoa msimamo wake katika mkutano wa mwisho wa mwaka kutokana na hapo awali kueleza bado anafikiria kwani hana jibu sahihi kwa wakati huo.

Monti anayeungwa mkono na viongozi wa Ulaya, wafanyabiashara na viongozi wa dini ameombwa na wafuasi wake kugombea ili kuinusuru Italia na mzozo wa kiuchumi.

Ikiwa atathibitisha kugombea katika uchaguzi mkuu ujao Monti atachuana na aliyekuwa waziri mkuu hapo kabla Silvio Berlusconi ambaye alijiuzulu mwaka uliopita kutokana na mzozo wa kiuchumi na kukosa uungwaji mkono baada ya bunge kupitisha mpango wa kubana matumizi uliotakiwa na umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.