Pata taarifa kuu
HISPANIA

Vyama vyenye ushawishi vyashinda nchini Hispania, wasiwasi wa kujitenga watanda

Vyama ambavyo vina ushawishi mkubwa nchini Uhispania na vinaungwa mkono na wananchi wengi katika Jimbo la Catalunya vimefanikiwa kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi ambao umefanyika hiyo jana.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Vyama hivyo ambavyo vimekuwa mstari wa mbele vikishinikiza kujitenga kwa Jimbo hilo vimefanikiwa kupata viti vingi katika uchaguzi huo kitu ambacho kinatajwa ni ishara ya kujitenga kwa Catalunya.

Wafuasi wa Vyama hivyo wameonekana kwenye mitaa mbalimbali ya Catalunya wakishangilia na kusema wakati wa ukombozi umefika na wanataka kujitenga kutoka katika serikali ya Uhispania.

Chama ambacho kilikuwa na nguvu kubwa katika Jimbo hilo kupitia Kiongozi wake Artur Mas kimeanza kusaka muungano ili kuhakikisha kinakuwa na nguvu katika kuendelea kutawala eneo hilo.

Iwapo vyama hivi viwili vitafanikiwa kuungana ni wazi kabisa kuna hatari kubwa ya Jimbo la Catalunya likajitenga kutoka katika serikali kuu ya Uhispani na mchakato wa kuwasilisha pendekezo hilo umeshaanza.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.