Pata taarifa kuu
Uswisi

Bado Wanawake duniani wanakabiliwa na Changamoto ya usawa kati yao na Wanaume katika Nyanja Mbalimbali

Hatua kubwa imepigwa na dunia kwa hivi sasa kuondoa utofauti wa kijinsia kati ya Wanawake na wanaume katika Maswala yahusuyo Afya na Elimu hata hivyo bado kuna kazi kubwa ya kupigania usawa katika Ajira za ngazi za juu na Mishahara, Ripoti ya utafiti uliofanywa kwatika nchi 135 duniani imeeleza.

Wanawake duniani wamekuwa wakihamasishana katika Maswala mbalimbali katika Jamii, ikiwemo suala la Usawa kijinsia
Wanawake duniani wamekuwa wakihamasishana katika Maswala mbalimbali katika Jamii, ikiwemo suala la Usawa kijinsia Divulgação Women's Forum
Matangazo ya kibiashara

Tofauti katika nafasi za juu za Ajira, Mshahara na ngazi ya Uongozi bado imeendelea kujionesha hata katika nchi zinazopigania usawa katika elimu na zile ambazo wanawake wameonekana kuwa na nafasi nzuri kiuchumi, Ripoti ya jukwaa la uchumi duniani WEF imeeleza katika Ripoti yake ya mwaka juu ya Maswala ya Utofauti wa kijinsia.
 

Ripoti hii imegusia zaidi ya asilimia 90 ya Idadi ya watu duniani ikiangalia namna ambavyo Mataifa yamekuwa yakigawa Rasilimali zake na Fursa miongoni mwa Wanawake na Wanaume.
 

Ripoti hiyo imeeleza kuwa nchi za Kaskazini mwa Ulaya na Atlantiki zinazoongozwa na Iceland, Finland na Norway wamefanya kazi nzuri katika kuweka hali sawa kati ya Wanawake na Wanaume kwenye suala la Ajira, huku Chad, Pakistan na Yemen wakiwa na Rekodi mbaya zaidi.
 

Katika eneo la kiuchumi imeelezwa kuwa wakati karibu nchi zote zimekuwa zikifanya jitihada katika kuweka hali ya usawa katika maswala ya Elimu na Afya, asilimia 60 pekee ya nchi hizo zinafanya vizuri katika kuondoa tofauti ya kiuchumi kati ya Wanawake na Wanaume na asilimia 20 wanafanya vizuri katika nyanja za kisiasa.
 

Miongoni mwa Nchi zinazofanya vizuri kiuchumi mwaka huu ni pamoja na Marekani, Japan na Ujerumani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.