Pata taarifa kuu
Ugiriki

Vyama vikuu vya wafanyakazi nchini Ugiriki vyatishia kuingia mgomoni Septemba 26

Vyama viwili vikuu vya Wafanyakazi nchini Ugiriki vimeitisha Mgomo tarehe 26 mwezi huu dhidi ya Hatua mpya za kubana matumizi, maafisa kutoka kwenye vyama hivyo wamethibitisha.

Maandamano ya wafanyakazi nchini Ugiriki
Maandamano ya wafanyakazi nchini Ugiriki
Matangazo ya kibiashara

chama cha Wafanyakazi wa Sekta Binafsi, GSSE na kile cha Uma, ADEDY kimeitisha Mgomo wa Saa 24 kupinga Mapngo mpya wa kubana Matumizi ulio mbioni kuanza kufanyiwa kazi na Serikali ya Nchi hiyo ili kupata Mkopo kutoka Umoja wa Ulaya EU na Shirika la Fedha duniani, IMF.

Ugiriki hivi sasa iko katika hati hati za mweishoni za kukamilisha Mchakato wa Kubana Matumizi ili kuokoa kiasi cha Euro Bilioni 11.5 ambazo zinahitajika ikiwa ni sharti ili kupata mkopo wa Euro Bilioni 31.

Wakaguzi wanaowakilisha Shirika la Fedha duniani , Umoja wa Ulaya na Benki kuu ya Ulaya wako jijini Athens nchini Ugiriki, wakijadili mpango wa kubana Matumizi na Serikali ya nchi hiyo.

Ripoti ya Wakaguzi hao inayotarajiwa kutolewa Mwezi Ujao, itatoa mwanga juu ya Ugiriki kupatiwa kitita hicho cha Fedha ili kuoakoa Uchumia wa Taifa hilo au la.

Mpango wa kubana matumizi umeelezwa kuathiri Pensheni, Gharama za Afya na kukatwa kwa kiasi cha Euro Milioni 517 katika Sekta ya Ulinzi. Mpango ambao umewaghadhabisha Raia wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.