Pata taarifa kuu
Italia-Uchumi

Waziri mkuu wa Italia azuru nchi kadhaa za ukanda wa Ulaya kujaribu kunusuru uchumi wa nchi yake

Waziri mkuu wa serikali ya Italia Mario Monti anataraji kuelekea jiji Madrid nchini Uhispania kukutana na mwenzie Mariano Rajoy wakati nchi hiyo nayo ikikabiliwa na tatizo la mdororo wa uchumi katika ukanda wa nchi zinazo tumia sarafu ya Ulaya.

Waziri mkuu wa Italia, Mario Monti
Waziri mkuu wa Italia, Mario Monti Reuters/Max Rossi
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili watakutana kwa mazungumzo na kufanya kazi kwa pamoja kabla ya kuendesha mkutano na vyombo vya habari. Waziri mkuu wa Italia atakutana pia na mfalme Juan Carlos.

Waziri mkuu Mario Monti, kabla ya kuzuru Uhispania, ataelekea pia jijini Paris siku ya Jumanne ambako atakutana na rais wa Ufaransa Francois Hollande na siku ya  Jumatano na alhamisi atatembelea nchini Finlande katika mazungumzo na mwenziwe Jyrki Katainen.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wameyahakikishia masoko ya Umoja huo kuhusu juhudi wanazo zifanya kuhakikisha uchumi wa nchi wanachama unaimarika na hivo kuepuka mporomoko wa kiuchumi.

Ujerumani na Italia zimekubaliana kufanya jitihada ziwezekanazo ili kulinda uchumi wa ukanda wa Euro.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.