Pata taarifa kuu
Iraq

Al Qaeda yakiri kuhusika na mashambulizi yaliyoua watu 113 nchini Iraq

Kundi la kigaidi la Al Qaeda limesema kuwa linahusika na wimbi la mashambulizi yaliyotokea siku kadhaa zilizopita na kuua watu wsiopungua 113 katika maeneo mbalimbali nchini humo.  

REUTERS/Imad al-Khozai
Matangazo ya kibiashara

 

Mashambulizi hayo yalizuka siku ya Jumatatu yalisababisha kujeruhiwa kwa watu wapatao 250 na yanaelezewa kuwa mabaya kuwahi kutokea katika siku za hivi karibuni.

Marekani kupitia kwa msemaji wa Ikulu ya Marekani Victoria Nuland imelaani vikali mashambulizi hayo ambayo yameongeza wasiwasi miongoni mwa raia wa Iraq.

Nuland amesema kuwa mashambulizi yanapaswa kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa kwa kuwa yalilenga raia wasio na hatia katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhan.

Mashambulizi hayo pia yamelaaniwa na vikali na nchi nyingine kama vile Marekani, Ufaransa, Canada na nchi jirani ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.