Pata taarifa kuu
Hague-ICC

Kiongozi wa Jeshi la waasi, Thomas Lubanga ahukumiwa kifungo cha miaka 14 na Mahakama ya ICC

Mahakama ya Uhalifu wa kivita ICC imemhukumu Kiongozi wa Jeshi la uasi, Thomas Lubanga kifungo cha miaka 14 jela hii leo kwa kosa la kutumia watoto katika Jeshi lake.

Kiongozi wa Jeshi la Waasi Thomas Lubanga
Kiongozi wa Jeshi la Waasi Thomas Lubanga REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Lubanga mwenye umri wa miaka 51 alipatikana na makosa na mahakama hiyo kwa kuwaajiri watoto wadogo katika kundi lake la waasi na kusababisha mauaji na vitendo vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu kati ya mwaka 2002 na 2003.

Mataifa sita yamekubali kumpa kifungo Lubanga ikiwemo Austria, Belgium, Britain, Finland, Mali na Serbia.

Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya ICC, Luis Moreno Ocampo,Mwanzoni mwa Mwezi huu alitoa wito Lubanga kuhukumiwa kifungo cha Miaka 30 kwa kile alichoeleza Makosa aliyoyafanya yanagusa Jamii ya Kimataifa.

Lubanga ambate amekuwa akishikiliwa Hague tangu Mwaka 2006 ni Mwanzilishi wa chama cha Union of Congolese Patriots,UPC na Kamanda wa Jeshi la Patriotic for the liberation of Congo (FPLC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.