Pata taarifa kuu
Uholanzi

Kiongozi wa Zamani wa Majeshi ya Serbia na Bosnia, Ratko Mladic afikishwa Mahakamani

Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Bosnia na Serbia Ratko Mladic hii leo amefikishwa mahakamani akishutumiwa kujihusisha na Mauaji ya Halaiki ambayo yanaelezwa kuwa mabaya zaidi tangu baada ya vita ya pili ya Dunia. 

Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Bosnia na Serbia, Ratko Mladic
Mkuu wa zamani wa Majeshi ya Bosnia na Serbia, Ratko Mladic REUTERS/Toussaint Kluiters
Matangazo ya kibiashara

Mladic 70, anakabilliwa na Mashtaka 11 ya mauaji ya Halaiki, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya Ubinaadam kwa kile kinachodaiwa kuhusika kwake na mauaji ya mwaka 1992-1995 ambapo watu laki moja walipoteza maisha na takriban watu 2.2 waliachwa bila makazi.
 

Mladic hakukutwa na hatia juu ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili wakati kesi yake iliposomwa mwezi Juni mwaka jana.
 

Hii leo nje ya Mahakama ya UN inayosikiliza kesi ya mauaji ya halaiki ya Srebrenica iliyo mjini Hague Uholanzi, kundi la wanawake takriban 25 wanaowakilisha Wajane na waliathiriwa na Mauaji hayo wamefanya maandamano.
 

Takriban Wanaume 8,000 na Wavulana waliuawa baada ya vikosi Vya Bosnia chini ya Amri ya Mladic.
 

Mladic atahukumiwa kifungo cha Maisha iwapo atakutwa na Hatia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.