Pata taarifa kuu
Uholanzi

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte ajiuzulu

Waziri mkuu wa Uholanzi Mark Ruttes toka chama cha Liberal ametangaza kujiuzulu kufuatia serikali yake kushindwa kuafikiana na vyama vya upinzani kuhusu mpango wa kubana matumizi. 

Mark Ruttes aliekuwa waziri mkuu wa Uholanzi ambae amejiuzulu
Mark Ruttes aliekuwa waziri mkuu wa Uholanzi ambae amejiuzulu le vif l'express
Matangazo ya kibiashara

Kujiuzulu kwa waziri mkuu huyo imekuwa ni pigo kwa serikali ya uholanzi ambayo ilikuwa inafanya juhudi kuhakikisha inawasilisha bajeti yake ya mpango wa kubana matumizi bungeni ili kuinusuru nchi hiyo kutumbukia kwenye matatizo ya kiuchumi.

Kwa majuma kadhaa sasa serikali ya Rutte ilikuwa kwenye shinikizo kubwa toka kwa vyama vingine vya mrengo wa kulia nchini humo waliokuwa wakipinga mpango huo wa serikali wakutaka kuwasilisha bajeti ya kubana matumizi.

Mpango wa kubana matumizi ambao ulikuwa uchukuliwe na serikali hiyo, ulikuwa ni moja ya mikakati yake katika kutimiza matakwa ya Umoja wa Ulaya kuhakikisha nchi zote za umoja huo zinabana matumizi kunusuru nchi zao kutumbukia kwenye mdororo wa uchumi.

Waziri mkuu huyo aliwasilisha baua yake ya kujiuzulu mchana wa jana baada ya kufanya mazungumzo na Beatrix ambaye ni malkia wa nchi hiyo kabla ya baadae kuthibitishwa kuwa Rutte aliwasilisha barua ya kujuzulu kwa baraza lake lote la mawaziri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.