Pata taarifa kuu
ARGENTINA-HISPANIA

Umoja wa Ulaya EU waionya nchi ya Argentina dhidi ya kutaifisha hisa za kampuni ya mafuta ya YPF

Serikali ya Argentina imeendeleza vita yake ya maneno na Uhispania wakati huu ambapo wakiendelea kuweka bayana wataendelea na mpango wao wa kutaifisha asilimia hamsini na moja za kampuni kongwe ya uzalishaji wa mafuta ya YPF. 

Visima vya mafuta mabavyo vinamilikiwa na kampuni ya YPF ya Uhispania
Visima vya mafuta mabavyo vinamilikiwa na kampuni ya YPF ya Uhispania Reuters
Matangazo ya kibiashara

Naibu Waziri wa Uchumi wa Argentina Axel Kicillof amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kampuni mama ya Repsol imeshindwa kusimamia vyema kampuni ya YPF ambayo imeshuhudiwa uzalishaji wake ukishuka kila kukicha.

Mgogoro huo wa kibiashara unaozigusa Argentina na Uhispania umegonga hodi kwenye Umoja wa Ulaya EU ambapo Mkuu wake wa sera za Kimataifa Catherine Ashton amelaani kitendo cha serikali ya Argentina.

Nchi wanachama za Umoja wa Ulaya EU zimekuwa mstari wa mbele kukosoa hatua ambayo imetengazwa na Argentina ya kutaka kutaifisha hisa za kampuni hiyo ya mafuta kwa zaidi ya asilimia 51 jambo ambalo linapingwa na Hispania.

Hapo jana serikali ya Hispania ilitangaza kuwa hatofumbia macho hatua zozote ambazo zitatangazwa na Argentina zitakazopelekea kutaifisha hisa hizo na kuwa italazimika kulinda maslahi ya nchi yake.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanadai kuwa hatua hiyo ya Argentina huenda ikaathiri uchumi wa taifa la Hispania ambalo kwa kiasi kikubwa pia imekuwa ikitegemea nishati ya mafuta ambayo inazalishwa na kampuni yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.