Pata taarifa kuu
ARGENTINA-HISPANIA

Nchi ya Hispania yaionya serikali ya Argentina endapo itadiriki kutaifisha hisa za kampuni yake ya mafuta ya YPF

Serikali ya Argentina imesema itataifisha asilimi hamsini na moja ya hisa za kampuni kubwa zaidi ya uzalishaji mafuta nchini humo ya YPF inayomilikiwa na Uhispania kitu ambacho kimeibua hasira kubwa kwa serikali ya Madrid ikipinga hatua hiyo. 

Waandamanaji nchini Argentina wakiunga mkono hatua ya serikali kutaifisha hisa za kampuni ya mafuta ya Hispania YPF
Waandamanaji nchini Argentina wakiunga mkono hatua ya serikali kutaifisha hisa za kampuni ya mafuta ya Hispania YPF Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Argentina Cristina Kirchner akishirikiana na Baraza la Mawaziri pamoja na Magavana wa nchini mwake ndiyo wametangaza uamuzi huo wakieleza hiyo ni sera yao mpya ya kutaifisha mali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.

Umoja wa Ulaya EU na serikali ya Uhispania kwa pamoja zimetoa onyo kwali kwa serikali ya Argentina ktotekeleza mpango wake lakini yenyewe imesema ni lazima ichukue asimilia hamsini na moja ya hisa hizo kwenye kampuni ya YPF.

Hatua ya Argentina kutishia kutaifisha hisa za kampuni hizo imechukuliwa kama kitendo cha uhujumu uchumi kwa nchi ya Hispania na kwamba haitokaa kimya endapo nchi hiyo itaamua kutekeleza azma yake.

Hatua ya nchi hiyo kutaka kutaifisha hisa za YPF inakuja kufuatia hivi karibuni kuibuka mvutano kati yake na serikali kuhusu kuongeza uzalishaji na kuhakikisha kuwa nchi ya Argentina inafaidika kutokana na uzalishaji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.