Pata taarifa kuu
UFARANSA

Sarkozy akanusha chama chake kujipatia fedha kinyume na taratibu

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ambaye pia anawania kutetea kiti chake, hii leo amekanusha vikali tuhuma zilizoelekezwa dhidi yake kuhusu chama chake kujipatia fedha kinyume cha sheria kwenye kampeni zake za urais mwaka 2007.

Matangazo ya kibiashara

Rais Sarkozy amekanusha chama chake kupata fedha hizo kinyume cha sheria toka kwa taasisi ya L'oreal na kuzitumia kwenye kampeni zake zilizomwezesha kushinda kiti cha urais.

Tuhuma hizo mpya dhidi ya Sarkozy zimetolewa na mgombea wa upinzani Francois Hollande ambaye amesema kitendo hicho kilifanyika kinyume cha sheria na kwamba kinastahili kuchunguzwa.

Kiasi cha euro laki nne kimeelezwa kuwa kilitolewa kwenye benki moja nchini Uswis kwaajili ya kuwezesha kampeni za kiongozi huyo.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa wagombea hao kuendelea kutupiana vijembe huku kila mmoja akilenga kujisafishia njia katika kinyang'anyiro.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.