Pata taarifa kuu
Ufaransa-Ugaidi

Kituo cha Televisheni cha Aljazeera kimesema hakitoonyesha picha za mashambulio ya Mohamed Merah

Televisheni ya Aljazeera imesema haitaonesha picha za mashambulio ya risasi aliyorekodi Mohamed Merah wakati akifanya mashambulio dhidi ya mwalimu na wanafunzi watatu wa shule ya kiyahudi mjini Toulouse. Familia za wahanga wa mauaji ya Toulouse na Montauban pamoja na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wameutaka uongozi wa kituo hicho kutopeperusha picha za video za mauaji hayo.

Nicolas Sarkozy Rais wa Ufaransa
Nicolas Sarkozy Rais wa Ufaransa REUTERS/Kenzo Tribouillard/Pool
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya televisheni hiyo iliyo jijini Paris imesema imepokea picha za video zinazoonesha mauaji ya watu hao na picha hizo zimekabidhiwa kwa polisi, lakini imesema haitaonesha picha hizo kwa kuwa ni kinyume na maadili ya chombo hicho.

Kabla ya kuuawa kwake Merah aliyekuwa na umri wa miaka 23 alirekodi picha wakati akitekeleza mauaji ya mwalimu, wanafunzi watatu na wanajeshi watatu.

Maafisa uchunguzi wanaamini kuwa Merah alikuwa akitekeleza mashambulio hayo peke yake hata hivyo inakisiwa kuwa huenda alikuwa akipata usaidizi kutoka kwa wengine akiwemo kaka yake ambaye anashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo kuna maswala ambayo yameibuka kuhusu nani aliepeleka picha hizo za video kwenye kituo cha Aljazeera Machi 23, siku ambayo pilisi ilikuwa imezingira nyumbani mwa Merah, wakati ndugu yake Abdelkader alikuw akihojiwa na polisi.

Polisi nchini Ufaransa wamesema, bila shaka kuna mtu mwingine watatu ambae alihusika na kurikodi video hiyo ambayo ilitengenezwa kikamilifu na kuchanganywa na muziki na sura za Qurani kwa kutumia kompyuta.

Katika hatua nyingine Baba wa Merah ametaka mwili wa Mwanae kusafirishwa mpaka Algeria kwa ajili ya Mazishi na amepanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya serikali ya Ufaransa kufuatia kifo cha mwanae, hatua ambayo Sarkozy ameiita ya kuhamaki.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.