Pata taarifa kuu
PAKISTAN-USWIS

Mahakama kuu nchini Pakistan yaagiza mamlaka nchini Uswis kufungua kesi za rushwa dhidi ya rais Zardari

Mahakama kuu nchini Pakistan imeagiza mamlaka nchini Uswis kufungua upya kesi za rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Serikali inayomkabili rais wa nchi hiyo Asif Ali Zardari. 

Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari
Rais wa Pakistan Asif Ali Zardari Reuters
Matangazo ya kibiashara

Amri hiyo ya mahakama inatolewa wakati kesi inayomkabili waziri mkuu Yousuf Raza Gilani ikiendelea kusikilizwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kushindwa kuwafungulia mashtaka viongozi wala rushwa.

Mahakama hiyo ilimfungulia kesi ya kukiuka katiba ya nchi hiyo kwa kushindwa kuwafungulia mashtaka rais Zardari pamoja na viongozi wengine wa Serikali ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya rushwa.

Mamlaka nchini Uswis ilitangaza kufuta kesi hizo kwa kile ilichoeleza ni maombi toka kwa Serikali ya Pakistan ambayo ilitaka kutofunguliwa mashtaka kwa aliyekuwa waziri mkuu Benazir Bhuto na rais wa sasa ambaye ni mmewe Asif Ali Zardari.

Waziri mkuu Gilani ameendelea kusisitiza kuwa hana hatia kuhusu mashtaka aliyofunguliwa na mahakama kuu na kwamba yeye anatekeleza kile ambacho kipo kwenye katiba kuhusu kuwafungulia mashtaka viongozi wa Serikali ambao kesi zao zilikiwishapita muda wake.

Kesi hiyo iliharishwa hadi tarehe 21 ya mwezi huu ambapo waziri mkuu Gilani anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kukiuka katiba ya nchi yanayomkabili.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.