Pata taarifa kuu
URUSI-UMOJA WA KIARABU

Viongozi wa Urusi na wale wa Umoja wa nchi za Kiarabu kukutana kuijadili Syria

Wakati mapigano yakiendelea kuripotiwa kwenye mji wa Homs nchini Syria, viongozi wa Urusi na wale wa Umoja wa nchi za Kiarabu wanatarajiwa kukutana mjini Cairo Misri tarehe kumi ya mwezi huu kujadili namna ya kutatua mgogoro wa Syria. 

Baadhi ya wanajeshi wa jeshi huru la Syria linalopigana na serikali
Baadhi ya wanajeshi wa jeshi huru la Syria linalopigana na serikali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari nchini Urusi vimemnukuu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye juma hili alikutana waziri wa mambo ya nje wa Jordan Nasser Judeh na kufanya nae mazungumzo kuhusu Syria.

Kwenye mkutano huo viongozi hao walijadili pamoja na mambo yahusuyo nchi zao lakini pia walizungumzia mgogoro wa Syria ambao umeendelea kukua na kusababisha maelfu ya wananchi kupoteza maisha kutokana na machafuko yanyoendelea.

Waziri Lavrov amesema kuwa ataandaa mkutano na viongozi wa Umoja wa nchi za Kirabu kwa lengo la kufanya mkutano wa pamoja kuangalia ni kwanamna gani wanaweza kushirikiana kupata suluhu ya mgogoro wa nchi hiyo.

Nchi ya Urusi imekuwa mstari wa mbele kupinga maazimio ya Umoja wa nchi za Kiarabu kuhusu kutatua mgogoro wa Syria ambapo imeendelea kusisitiza kuwa nguvu za kijesh hazitaweza kumaliza mzozo unaoendelea nchini humo.

Mataifa ya Magharibi yamekuwa yakilaani hatua ya Urusi na China kuendelea kutumia kura yao ya turufu kuzuia maazimio ambayo yanataka kupitishwa na nchi hizo kwaajili kushinikiza kuchukuliwa hatua kali dhidi ya serikali ya Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.