Pata taarifa kuu
Ujerumani

Rais wa Ujerumani ajiuzulu kutokana na kashifa

Rais wa Ujerumani Christian Wulff ametangaza kujiuzulu kutokana na kukabiliwa na kashifa ya mkopo wa nyumba alioukubali wakati akiwa mkuu wa taasisi moja.Kufuatia taarifa ya kujiuzulu kwa Bwana Wulff, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameahirisha safari yake ya Italia ambako alipaswa kutembelea ikiwa ni harakati za kushughulikia mgogoro wa kiuchumi.

REUTERS/Tobias Schwarz/Files
Matangazo ya kibiashara

Kansela Angela Merkel alipaswa kufanya ziara yake hiyo leo na amesema amehudhunishwa na hatua ya Rais Wulff na ameelezea kujuta kwake kutokana na hatua hiyo iliyochukuliwa na kiongozi huyo.

Bwana Wulff amesema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo kwa kuwa anaamini alifanya kazi kwa uaminifu na kwa maslahi ya taifa na wananchi wa Ujerumani.

Kansela Merkel amekubali kujiuzulu kwa Rais huyo na kusema kuwa katika muda wake ofisini alifanya kwa kwa kujitoa kwa kuangalia na kuweka mbele maslahi ya Ujerumani.

Merkel alipambana kwa kiasi kikubwa kuhakikisha Bwana Wulff anateuliwa kuwa Rais kupitia chama cha mrengo wa kati kulia, CDU na vyama vya siasa vitawajibika kukubaliana ili kupata mtu atakayechukua nafasi ya Rais huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.