Pata taarifa kuu

Kiongozi wa Afghanistan ametoa wito wa kuheshimiwa kwa sharia

Nairobi – Kiongozi wa serikali ya Afghanistan katika ujumbe wake kuelekea kumalizika kwa mfungo mwa mwezi wa Ramadan, amewataka raia kwenye taifa hilo kuheshimu kanuni za sharia ambapo pia ametoa wito wa kuwepo kwa uhusiano mwema na jamii ya kimataifa.

Serikali ya Taliban haitambuliwi kimataifa.
Serikali ya Taliban haitambuliwi kimataifa. AP - Siddiqullah Alizai
Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe wake kuelekea sherehe za Eid al-Fitr wiki ijayo, Hibatullah Akhundzada, amesema kutokwepo kwa haki na kwenda kinyume na sharia kunasababisha kuendelea kuwepo kwa utovu wa usalama.

Tangu kurejea madarakani mwezi Agosti mwaka wa 2021, utawala wa Taliban umekuwa ukishinikiza utekelezwaji kikamilifu wa sharia za kiisilamu.

Wanawake ni miongoni mwa walioathirika zaidi na kanuni hizo ambazo zimewafanya baadhi kuhofia kutembea hadharani.

Serikali ya Taliban haitambuliwi kimataifa ambapo ujumbe wa Hibatullah haukugusia masuala muhimu likiwemo suala la kidiplomasia pamoja na iwapo itawaruhusu wanawake na wasichana kurejea shuleni na vyuo vikuu.

Katika kipindi cha kwanza cha utawala wa Taliban, kulikuwepo na visa vya watu kuwanyongwa hadharani baadhi ya visa hivyo vikiripotiwa tangu Taliban kurejea uongozini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.