Pata taarifa kuu

Baraza la usalama la UN limepiga kura kuzuia uuzaji wa silaha kwa Israeli

Nairobi – Baraza la usalama katika Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kusitishwa kwa uuzaji wa silaha za aina yoyote kwa Israeli.

Israeli imeendeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza ikisema kuwa inawasaka wapiganaji wa Hamas
Israeli imeendeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza ikisema kuwa inawasaka wapiganaji wa Hamas AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa baraza hilo, hatua hii imechukuliwa kutokana na kile ambacho kimetajwa kama uwezekano wa Israeli kutekeleza mauaji ya kimbari katika vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza.

Kwa sasa watu zaidi ya elfu 30 wameripotiwa kuuawa katika mashambulio ya Israeli katika ukanda wa Gaza.

Azimio hilo limeungwa mkono na nchi wanachama 28 kati ya 47, nchi sita zipinga azimio hilo wakati nyengine 13 zikijizuia kupiga kura.

Israeli imekuwa ikituhumiwa kwa kutekeleza mauaji ya halaiki katika ukanda wa Gaza
Israeli imekuwa ikituhumiwa kwa kutekeleza mauaji ya halaiki katika ukanda wa Gaza REUTERS - Dawoud Abu Alkas

Hii ni mara ya kwanza kwa baraza hilo la UN kuchukua msimamo kuhusu kinachoendelea katika Ukanda wa Gaza.

Haya yanajiri wakati huu rais wa Marekani, Joe Biden, akiionya Israel dhidi ya kile alichosema huenda akabadili sera yake kuhusu mzozo wa Gaza, wakati huu akionesha kutoridhishwa na namna waziri mkuu Benjamin Netanyahu, anashughulikia mwito wa kuwalinda raia.

Marekani ni mshirika wa karibu wa Israeli
Marekani ni mshirika wa karibu wa Israeli © Miriam Alster / AP

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, anasema rais Biden huenda akasitisha au kupunguza msaada wake kwa Israel, ikiwa raia wataendelea kuuawa kiholela.

Onyo la Biden, nalo pia limekuja wakati huu jumuiya ya kimataifa ikiongeza shinikizo kwa Israel kusitisha vita na kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.