Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza: Jeshi la Israeli linaedesha operesheni kubwa kwenye hospitali ya al-Shifa

Jeshi la Israel limetangaza leo Jumatatu Machi 18 kwamba limekuwa likifanya operesheni kwenye hospitali ya al-Shifa. Hospitali kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza, iliyoko kaskazini mwa eneo hilo, inawaficha maafisa wa Hamas, kulingana na Israeli.

Muonekano wa nje wa hospitali ya al-Shifa katika Ukanda wa Gaza, hapa ilikuwa tarehe 10 Novemba 2023.
Muonekano wa nje wa hospitali ya al-Shifa katika Ukanda wa Gaza, hapa ilikuwa tarehe 10 Novemba 2023. © ISMAIL ZANOUN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Ni operesheni ambayo ilianza usiku wa manane dhidi ya hospitali hii, kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza, ya kwanza kulengwa mwezi uliopita wa Novemba na wanajeshi wa Israel. Operesheni ndogo, kulingana na msemaji wa jeshi la Israeli Jenerali Daniel Hagari: "IDF inaendesha operesheni ya usahihi wa hali ya juu katika maeneo machache ya hospitali ya al-Shifa. Hii inafuatia taarifa thabiti za kiintelijensia ambazo zinahitaji hatua za haraka. Tunajua kwamba magaidi wakuu wa Hamas wamekusanyika katika hospitali hiyo na wanaitumia kuendesha operesheni dhidi ya Israel. "

Wakati huo huo, mashahidi wanaripoti mashambulio ya angani kwenye wilaya ya Al-Rimal ambapo hospitali hii inapatikana ambapo, kulingana na vyanzo vya Palestina, imezingirwa na vifaru vya kijeshi vya Israel. Pia kuna taarifa za majibizano ya urushianji risasi ndani ya uwanja wa hospitali. Wizara ya Afya katika Gaza inayodhibitiwa na Hamas inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati kukomesha kile kinachotajwa kuwa mauaji.

Usitishwaji wa mapigano kuzingatiwa?

Wakati huo huo, ujumbe wa Israel hatimaye utaanza tena mazungumzo ya usitishwaji vita na kubadilishana mateka na wafungwa wa Kipalestina. Mjadala mgumu juu ya hali ngumu. Baraza la mawaziri la vita na baraza pana la mawaziri la usalama wameidhinisha kuanzishwa tena kwa mazungumzo huko Doha, Qatar.

Katika saa zijazo, wajumbe wa Israel watasafiri kwenda Qatar. Ujumbe wa israel unaongozwa na mkuu wa Mossad David Barnea na atakuwa na uwezo wa kukamilisha makubaliano kwa misingi ya mapendekezo ya Hamas ambayo, Waisraeli wanasema, ni mabaya, lakini yanatoa msingi unaowezekana wa mazungumzo. "Ni vigumu kusema kwamba tuna matumaini," kimesema chanzo cha kisiasa cha Israel leo Jumatatu asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.